Follow Us:

MAJUKUMU YA KURUGENZI ZA TISTA?

(A) KURUGENZI YA MITAALA 1. Kubuni na kukuza mitaala katika ngazi ya elimu ya awali, elimu ya msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu.
2. Kubuni na kukuza mitaala ya Madarasa kwa watoto, vijana na watu wazima.
3. Kuandaa na kuendesha mitihani ya Taifa ya somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa wahitimu wa shule ya msingi.
4. Kuandaa na kuendesha mtihani wa taifa wa Madrasa.
(B) KURUGENZI YA TEHAMA
1. Kuanzisha na kuendesha tovuti ya TISTA.
2. Kusimamia mifumo ya kompyuta na kusanikisha program za TISTA.
3. Kusanikisha, kuweka na kubuni teknolojia mpya ya huduma ya mawasiliano.
4. Kutunza data za TISTA katika mifumo ya kidijitali na iliyo salama.
5. Kutoa mafunzo kwa wanafunzi na walimu kwa njia ya mtandao.
(C) KURUGENZI YA MAFUNZO NA URATIBU
1. Kuratibu ufundishaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu.
2. Kuratibu Program za walimu Waislamu.
3. Kuratibu kambi za wahitimu wa kidato cha nne.
4. Kuendesha warsha na semina za walimu.
5. Kuratibu program za wanafunzi.
6. Kuratibu ufundishaji wa Madrasa za mtaala.
Wanafunzi Wakiwa ktk Moja ya Kambi Iringa 2024.
(D) KURUGENZI YA TAKWIMU
1. Kukusanya takwimu za somo la EDK kuhusiana na idadi ya wanafunzi, idadi ya walimu waliopo, viwango vya ufaulu n.k
2. Kuchakata takwimu za somo la EDK na kupata uhitaji wa walimu, vitabu na vitendea kazi vingine.
3. Kukusanya takwimu zingine Muhimu kwa ajili ya Program za TISTA.
(E) KURUGENZI YA MAWASILIANO NA ELIMU KWA UMMAH
Ni kiunganishi cha Viongozi, Idara na Wadau Wote.
Kuhamasisha Ufikiaji wa Malengo.
Kutoa Taarifa za TISTA kwa Walengwa.
Kufuatilia na Kusahihisha Upotoshaji juu ya TISTA na Program zake.
5. Kuimarisha Mahusiano na Wadau.
6. Kuratibu Matukio ya Ndani na ya Nje ya TISTA.
7. Na jukumu jingine lolote litakalohusika na Idara hii.
(F). KURUGENZI YA UCHUMI NA FEDHA
Kuandaa na kusimamia kanuni za Fedha.
Kufanya Makisio ya Mapato na Matumizi.
Kubuni vyanzo vya Mapato na Ukusanyaji wake.
Kusimamia Matumizi ya Fedha kwa mujibu wa Kanuni.
Kutunza kumbukumbu za Fedha na Kutoa taarifa za Fedha kwa Wadau wa TISTA.
Wadau wa TISTA ni pamoja na Taasisi na Jumuiya zote za Kiislamu, Waislamu mmoja mmoja na Wazazi.